Site uses cookies to provide basic functionality.

OK
I TIMOTHY
1 2 3 4 5 6
Prev Up Next Toggle notes
Chapter 2
I Ti Swahili 2:1  Kwanza kabisa, basi naomba dua, sala, maombi na sala za shukrani zitolewe kwa Mungu kwa ajili ya watu wote,
I Ti Swahili 2:2  kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amani pamoja na uchaji wa Mungu na mwenendo mwema.
I Ti Swahili 2:3  Jambo hili ni jema na lampendeza Mungu Mwokozi wetu,
I Ti Swahili 2:4  ambaye anataka watu wote waokolewe na wapate kuujua ukweli.
I Ti Swahili 2:5  Maana yuko Mungu mmoja, na pia yuko mmoja anayewapatanisha watu na Mungu, binadamu Kristo Yesu,
I Ti Swahili 2:6  ambaye alijitoa mwenyewe kuwakomboa watu wote. Huo ulikuwa uthibitisho, wakati ufaao ulipowadia.
I Ti Swahili 2:7  Kwa sababu hiyo mimi nilitumwa niwe mtume na mwalimu wa watu wa mataifa, niutangaze ujumbe wa imani na ukweli. Nasema ukweli; sisemi uongo!
I Ti Swahili 2:8  Basi, popote mnapokutana kufanya ibada nataka wanaume wasali, watu waliojitolea kweli na ambao wanaweza kuinua mikono yao wakisali bila hasira wala ubishi.
I Ti Swahili 2:9  Hali kadhalika, nawataka wanawake wawe wanyofu na wenye busara kuhusu mavazi yao; wavae sawasawa na si kwa urembo wa mitindo ya kusuka nywele, kujipamba kwa dhahabu, lulu au mavazi ya gharama kubwa,
I Ti Swahili 2:10  bali kwa matendo mema kama iwapasavyo wanawake wamchao Mungu.
I Ti Swahili 2:11  Wanawake wanapaswa kukaa kimya na kuwa wanyenyekevu wakati wa kujifunza.
I Ti Swahili 2:12  Mimi simruhusu mwanamke amfundishe au amtawale mwanamume; anapaswa kukaa kimya.
I Ti Swahili 2:14  Na wala si Adamu aliyedanganywa; bali mwanamke ndiye aliyedanganywa, akaivunja sheria ya Mungu.
I Ti Swahili 2:15  Hata hivyo, mwanamke ataokolewa kwa kupata watoto, kama akidumu katika imani, upendo, utakatifu na unyofu.