Site uses cookies to provide basic functionality.

OK
REVELATION OF JOHN
Prev Up Next Toggle notes
Chapter 11
Reve Swahili 11:1  Kisha nikapewa mwanzi uliokuwa kama kijiti cha kupimia, nikaambiwa, "Inuka, ukalipime Hekalu la Mungu, madhabahu ya kufukizia ubani, na ukawahesabu watu wanaoabudu ndani ya Hekalu.
Reve Swahili 11:2  Lakini uache ukumbi ulio nje ya Hekalu; usiupime, maana huo umekabidhiwa watu wa mataifa mengine, ambao wataukanyanga mji Mtakatifu kwa muda wa miezi arobaini na miwili.
Reve Swahili 11:3  Nami nitawatuma mashahidi wangu wawili ili watangaze ujumbe wa Mungu kwa muda huo wa siku elfu moja mia mbili na sitini wakiwa wamevaa mavazi ya magunia."
Reve Swahili 11:4  Hao mashahidi wawili ni miti miwili ya Mizeituni na taa mbili zinazosimama mbele ya Bwana wa dunia.
Reve Swahili 11:5  Kama mtu akijaribu kuwadhuru, moto hutoka kinywani mwao na kuwaangamiza adui zao; na kila mtu atakayejaribu kuwadhuru atakufa namna hiyo.
Reve Swahili 11:6  Hao wanayo mamlaka ya kufunga anga, mvua isinyeshe wakati wanapotangaza ujumbe wa Mungu. Tena wanayo mamlaka ya kuzigeuza chemchemi zote za maji ziwe damu, na ya kusababisha maafa ya kila namna duniani kila mara wapendavyo.
Reve Swahili 11:7  Lakini wakisha maliza kutangaza ujumbe huo, mnyama atokaye shimoni kuzimu atapigana nao, atawashinda na kuwaua.
Reve Swahili 11:8  Maiti zao zitabaki katika barabara za mji mkuu ambapo Bwana wao alisulubiwa; jina la kupanga la mji huo ni Sodoma au Misri.
Reve Swahili 11:9  Watu wa kila kabila, lugha, taifa na rangi wataziangalia maiti hizo kwa muda wa siku tatu na nusu, na hawataruhusu zizikwe.
Reve Swahili 11:10  Watu waishio duniani watafurahia kifo cha hao wawili. Watafanya sherehe na kupelekeana zawadi maana manabii hawa wawili walikuwa wamewasumbua mno watu wa dunia.
Reve Swahili 11:11  Lakini baada ya zile siku tatu na nusu pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu iliwaingia, nao wakasimama; wote waliowaona wakaingiwa na hofu kuu.
Reve Swahili 11:12  Kisha hao manabii wawili wakasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikiwaambia, "Njoni hapa juu!" Nao wakapanda juu mbinguni katika wingu, maadui wao wakiwa wanawatazama.
Reve Swahili 11:13  Wakati huohuo, kukatokea tetemeko kubwa la ardhi, sehemu moja ya kumi ya ardhi ikaharibiwa. Watu elfu saba wakauawa kwa tetemeko hilo la ardhi. Watu waliosalia wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.
Reve Swahili 11:14  Maafa ya pili yamepita; lakini tazama! Maafa ya tatu yanafuata hima.
Reve Swahili 11:15  Kisha malaika wa saba akapiga tarumbeta yake. Na sauti kuu zikasikika mbinguni zikisema, "Sasa utawala juu ya ulimwengu ni wa Bwana wetu na Kristo wake. Naye atatawala milele na milele!"
Reve Swahili 11:16  Kisha wale wazee ishirini na wanne walioketi mbele ya Mungu katika viti vyao vya enzi, wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu,
Reve Swahili 11:17  wakisema: "Bwana Mungu Mwenye uwezo, uliyeko na uliyekuwako! Tunakushukuru, maana umetumia nguvu yako kuu ukaanza kutawala!
Reve Swahili 11:18  Watu wa mataifa waliwaka hasira, maana wakati wa ghadhabu yako umefika, wakati wa kuwahukumu wafu. Ndio wakati wa kuwatuza watumishi wako manabii, watu wako na wote wanaolitukuza jina lako, wakubwa kwa wadogo. Ni wakati wa kuwaangamiza wale wanaoangamiza dunia."
Reve Swahili 11:19  Hekalu la Mungu mbinguni likafunguliwa, na Sanduku la Agano lake likaonekana Hekaluni mwake. Kisha kukatokea umeme, sauti, ngurumo, tetemeko la ardhi, na mvua kubwa ya mawe.