Site uses cookies to provide basic functionality.

OK
GALATIANS
1 2 3 4 5 6
Prev Up Next Toggle notes
Chapter 5
Gala Swahili 5:1  Kristo alitupa uhuru akataka tubaki huru. Basi, simameni imara wala msikubali tena kuwa chini ya nira ya utumwa.
Gala Swahili 5:2  Sikilizeni! Ni mimi Paulo ninayesema nanyi! Kama mkikubali kutahiriwa, Kristo hatawafaidia chochote.
Gala Swahili 5:3  Nasema tena wazi: kila anayekubali kutahiriwa itambidi kuishika Sheria yote.
Gala Swahili 5:4  Kama mnatazamia kukubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya Sheria, basi, mmejitenga mbali na Kristo; mko nje ya neema ya Mungu.
Gala Swahili 5:5  Kwa upande wetu, lakini, sisi tunatumaini kwamba kwa nguvu ya Roho tunakubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya imani.
Gala Swahili 5:6  Maana ikiwa tumeungana na Kristo Yesu, kutahiriwa au kutotahiriwa hakuna maana; cha maana ni imani ifanyayo kazi kwa mapendo.
Gala Swahili 5:7  Mwenendo wenu ulikuwa mzuri! Nani, basi aliyewazuia kuuzingatia ukweli?
Gala Swahili 5:8  Aliyesababisha hali hiyo si Mungu ambaye amewaiteni.
Gala Swahili 5:9  "chachu kidogo tu huchachusha donge lote la unga!"
Gala Swahili 5:10  Kutokana na kuungana kwetu na Bwana, nina tumaini kubwa kwamba ninyi hamtakuwa na msimamo tofauti nami. Tena yeyote huyo anayewavurugeni--awe nani au nani--hakika ataadhibiwa.
Gala Swahili 5:11  Na kwa upande wangu, ndugu zangu, kama bado ninahubiri kwamba kutahiriwa ni lazima, kwa nini basi, bado ninadhulumiwa? Kama ingalikuwa hivyo, mahubiri yangu juu ya msalaba wa Kristo yasingalileta aibu yoyote.
Gala Swahili 5:12  Laiti hao wanaowavurugeni wangejikatakata wenyewe!
Gala Swahili 5:13  Ninyi, ndugu, mliitwa muwe watu huru. Lakini uhuru huo usiwe kisingizio cha kutawaliwa na tamaa za kidunia; ila mnapaswa kutumikiana kwa upendo.
Gala Swahili 5:14  Maana Sheria yote hutimizwa katika kushika amri hii moja: "Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe."
Gala Swahili 5:15  Lakini ikiwa mtaumana na kutafunana kama wanyama, jihadharini msije mkaangamizana wenyewe kwa wenyewe!
Gala Swahili 5:16  Basi, nasema hivi: mwenendo wenu na uongozwe na Roho, nanyi hamtafuata tena tamaa za kidunia.
Gala Swahili 5:17  Maana, tamaa za kidunia hupingana na matakwa ya Roho; na matakwa ya Roho hupingana na tamaa za kidunia. Mambo hayo mawili hayaafikiani; kwa sababu hiyo hamwezi kufanya yale mnayotaka ninyi wenyewe.
Gala Swahili 5:18  Kama mkiongozwa na Roho, basi, hamko tena chini ya Sheria.
Gala Swahili 5:19  Basi, matendo ya kidunia yanajulikana: uzinzi, uasherati, ufisadi;
Gala Swahili 5:20  kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, choyo, mabishano, mafarakano;
Gala Swahili 5:21  husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine kama hayo. Nawaambieni tena kama nilivyokwisha sema: watu wanaotenda mambo hayo hawatakuwa na nafasi yao katika ufalme wa Mungu.
Gala Swahili 5:22  Lakini matokeo ya kuongozwa na Roho ni mapendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu,
Gala Swahili 5:23  upole na kuwa na kiasi. Hakuna Sheria inayoweza kupinga mambo hayo.
Gala Swahili 5:24  Wale walio wa Kristo wameisulubisha hali yao ya kidunia pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.
Gala Swahili 5:25  Tukiishi kwa msaada wa Roho, na tuufuate mwongozo wake.
Gala Swahili 5:26  Basi, tusijivune, tusichokozane wala kuoneana wivu.