Site uses cookies to provide basic functionality.

OK
MARK
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16
Prev Up Next Toggle notes
Chapter 13
Mark Swahili 13:1  Yesu alipokuwa anatoka Hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake alimwambia, "Mwalimu, tazama jinsi mawe haya na majengo haya yalivyo ya ajabu!"
Mark Swahili 13:2  Yesu akamwambia, "Je, unayaona majengo haya makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalosalia juu ya lingine; kila kitu kitabomolewa."
Mark Swahili 13:3  Yesu alipokuwa ameketi juu ya mlima wa Mizeituni akielekea Hekalu, Petro, Yakobo, Yohane na Andrea wakamwuliza kwa faragha,
Mark Swahili 13:4  "Twambie mambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonyesha kwamba mambo haya karibu yatimizwe?"
Mark Swahili 13:5  Yesu akaanza kuwaambia, "Jihadharini msije mkadanganywa na mtu.
Mark Swahili 13:6  Maana wengi watakuja wakilitumia jina langu, wakisema, Mimi ndiye! nao watawapotosha watu wengi.
Mark Swahili 13:7  Mtakaposikia juu ya vita na fununu za vita, msifadhaike. Mambo hayo lazima yatokee, lakini mwisho wenyewe ungali bado.
Mark Swahili 13:8  Taifa moja litapigana na taifa lingine; utawala mmoja utapigana na utawala mwingine; kila mahali kutakuwa na mitetemeko ya ardhi na njaa. Mambo haya ni kama tu maumivu ya kwanza ya kujifungua mtoto.
Mark Swahili 13:9  "Lakini ninyi jihadharini. Maana watu watawapelekeni mahakamani, na kuwapigeni katika masunagogi. Mtapelekwa mbele ya watawala na wafalme kwa sababu yangu ili mpate kunishuhudia kwao.
Mark Swahili 13:10  Lakini lazima kwanza Habari Njema ihubiriwe kwa mataifa yote.
Mark Swahili 13:11  Nao watakapowatieni nguvuni na kuwapeleka mahakamani, msiwe na wasiwasi juu ya yale mtakayosema; saa ile itakapofika, semeni chochote mtakachopewa, maana si ninyi mtakaosema, bali Roho Mtakatifu.
Mark Swahili 13:12  Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe; baba atamsaliti mwanae; watoto watawashambulia wazazi wao na kuwaua.
Mark Swahili 13:13  Watu wote watawachukieni ninyi kwa sababu ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokolewa.
Mark Swahili 13:14  "Mtakapoona Chukizo Haribifu limesimama mahali ambapo si pake, (msomaji na atambue maana yake!) Hapo watu walioko Yudea wakimbilie milimani.
Mark Swahili 13:15  Mtu aliye juu ya paa la nyumba asishuke kuingia nyumbani mwake kuchukua kitu.
Mark Swahili 13:18  Ombeni ili mambo hayo yasitukie nyakati za baridi.
Mark Swahili 13:19  Maana wakati huo kutakuwa na dhiki ambayo haijatokea tangu Mungu alipoumba ulimwengu mpaka leo, wala haitatokea tena.
Mark Swahili 13:20  Kama Bwana asingepunguza siku hizo, hakuna binadamu ambaye angeokolewa. Lakini kwa ajili ya wateule wake, Bwana amezipunguza siku hizo.
Mark Swahili 13:21  "Basi mtu akiwaambieni, Tazama, Kristo yupo hapa! au Yupo pale! msimsadiki.
Mark Swahili 13:22  Maana watatokea kina Kristo wa uongo na manabii wa uongo, watafanya ishara na maajabu, ili kuwapotosha wateule wa Mungu, kama ikiwezekana.
Mark Swahili 13:23  Lakini ninyi jihadharini. Mimi nimewaambieni mambo yote kabla hayajatokea.
Mark Swahili 13:24  "Basi, siku hizo baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza na mwezi hautaangaza.
Mark Swahili 13:25  Nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbingu zitatikiswa.
Mark Swahili 13:26  Hapo watamwona Mwana wa Mtu akija katika mawingu kwa nguvu nyingi na utukufu.
Mark Swahili 13:27  Kisha atawatuma malaika wake; atawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho wa dunia mpaka mwisho wa mbingu.
Mark Swahili 13:28  "Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.
Mark Swahili 13:29  Hali kadhalika nanyi mtakapoona mambo hayo yakitendeka, jueni kwamba Mwana wa Mtu yuko karibu sana.
Mark Swahili 13:30  Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo hayo yote kutukia.
Mark Swahili 13:31  Mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Mark Swahili 13:32  "Lakini hakuna mtu ajuaye siku au saa hiyo itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye.
Mark Swahili 13:33  Muwe waangalifu na kesheni, maana hamjui wakati huo utafika lini.
Mark Swahili 13:34  Itakuwa kama mtu anayeondoka nyumbani kwenda safari akiwaachia watumishi wake madaraka, kila mmoja na kazi yake; akamwambia mlinzi wa mlango awe macho.
Mark Swahili 13:35  Kesheni, basi, kwa maana hamjui mwenye nyumba atarudi lini; huenda ikawa jioni, usiku wa manane, alfajiri au asubuhi.
Mark Swahili 13:36  Kesheni ili akija ghafla asije akawakuta mmelala.