Site uses cookies to provide basic functionality.

OK
MARK
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16
Prev Up Next Toggle notes
Chapter 10
Mark Swahili 10:1  Yesu alitoka hapo akaenda mkoani Yudea na hata ng'ambo ya mto Yordani. Umati wa watu ukamwendea tena, naye akawafundisha tena kama ilivyokuwa desturi yake.
Mark Swahili 10:2  Basi, Mafarisayo wakamwendea, na kwa kumjaribu wakamwuliza, "Je, ni halali mtu kumpa talaka mkewe?"
Mark Swahili 10:4  Nao wakasema, "Mose aliagiza mume kumpatia mkewe hati ya talaka na kumwacha."
Mark Swahili 10:5  Yesu akawaambia, "Mose aliwaandikia amri hiyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu.
Mark Swahili 10:6  Lakini tangu kuumbwa ulimwengu, Mungu aliumba mwanamume na mwanamke.
Mark Swahili 10:7  Hivyo mwanamume atawaacha baba yake na mama yake, ataungana na mkewe,
Mark Swahili 10:8  nao wawili watakuwa mwili mmoja. Kwa hiyo, wao si wawili tena bali mwili mmoja.
Mark Swahili 10:9  Basi, alichounganisha Mungu, binadamu asitenganishe."
Mark Swahili 10:10  Walipoingia tena ndani ya nyumba, wanafunzi wake walimwuliza juu ya jambo hilo.
Mark Swahili 10:11  Naye akawaambia, "Anayemwacha mkewe na kuoa mwingine, anazini dhidi ya mkewe.
Mark Swahili 10:12  Na mwanamke anayemwacha mumewe na kuolewa na mwingine anazini."
Mark Swahili 10:13  Watu walimletea Yesu watoto wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wakawakemea.
Mark Swahili 10:14  Yesu alipoona hivyo, alikasirika akawaambia, "Waacheni hao watoto waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni kwa ajili ya watu walio kama watoto hawa.
Mark Swahili 10:15  Nawaambieni kweli, mtu yeyote asiyeupokea Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hataingia katika Ufalme huo."
Mark Swahili 10:16  Kisha akawapokea watoto hao, akawawekea mikono, akawabariki.
Mark Swahili 10:17  Yesu alipoanza tena safari yake, mtu mmoja alimjia mbio, akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, "Mwalimu mwema, nifanyeje ili niupate uzima wa milele?"
Mark Swahili 10:18  Yesu akamjibu, "Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila Mungu peke yake.
Mark Swahili 10:19  Unazijua amri: Usizini; Usiue; Usiibe; Usitoe ushahidi wa uongo; Usidanganye; Waheshimu baba na mama yako."
Mark Swahili 10:20  Naye akamjibu, "Mwalimu, hayo yote nimeyazingatia tangu ujana wangu."
Mark Swahili 10:21  Yesu akamtazama, akampenda, akamwambia, "Umepungukiwa na kitu kimoja: nenda ukauze vitu ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate."
Mark Swahili 10:22  Aliposikia hayo, alisikitika, akaenda zake akiwa na huzuni, kwa maana alikuwa na mali nyingi.
Mark Swahili 10:23  Yesu akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, "Jinsi gani itakavyokuwa vigumu kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu!"
Mark Swahili 10:24  Wanafunzi walishangazwa na maneno yake. Yesu akawaambia tena, "Watoto wangu, ni vigumu sana kuingia katika Ufalme wa Mungu!
Mark Swahili 10:25  Ni rahisi zaidi ngamia kupenya katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu."
Mark Swahili 10:26  Wanafunzi wake wakashangaa sana wakaulizana, "Ni nani basi, atakayeweza kuokoka?"
Mark Swahili 10:27  Yesu akawatazama, akawaambia, "Kwa binadamu haiwezekani, lakini kwa Mungu si hivyo, maana kwa Mungu mambo yote huwezekana."
Mark Swahili 10:28  Petro akamwambia, "Na sisi je? Tumeacha yote, tukakufuata!"
Mark Swahili 10:29  Yesu akasema, "Kweli nawaambieni, kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu, au dada, au mama, au baba, au watoto au mashamba kwa ajili yangu na kwa ajili ya Habari Njema,
Mark Swahili 10:30  atapokea mara mia zaidi wakati huu wa sasa nyumba, ndugu, dada, mama, watoto na mashamba pamoja na mateso; na katika wakati ujao atapokea uzima wa milele.
Mark Swahili 10:31  Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza."
Mark Swahili 10:32  Basi, walikuwa njiani kwenda Yerusalemu, na Yesu alikuwa anawatangulia. Wanafunzi wake walijawa na hofu, na watu waliofuata waliogopa. Yesu akawachukua tena kando wale kumi na wawili, akaanza kuwaambia yale yatakayompata:
Mark Swahili 10:33  "Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu, na huko Mwana wa Mtu atakabidhiwa kwa makuhani wakuu na walimu wa Sheria, nao watamhukumu auawe na kumkabidhi kwa watu wa mataifa.
Mark Swahili 10:34  Nao watamdhihaki; watamtemea mate, watampiga mijeledi na kumwua. Na baada ya siku tatu atafufuka."
Mark Swahili 10:35  Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, "Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba."
Mark Swahili 10:37  Wakamjibu, "Uturuhusu tuketi mmoja upande wako wa kulia na mwingine upande wako wa kushoto katika utukufu wa Ufalme wako."
Mark Swahili 10:38  Yesu akawaambia, "Hamjui mnachoomba! Je, mnaweza kunywa kikombe nitakachokunywa, au kubatizwa kama nitakavyobatizwa?"
Mark Swahili 10:39  Wakamjibu, "Tunaweza." Yesu akawaambia, "Kikombe nitakachokunywa mtakinywa kweli, na mtabatizwa kama nitakavyobatizwa.
Mark Swahili 10:40  Lakini ni nani atakayeketi kulia au kushoto kwangu si wajibu wangu kupanga, bali nafasi hizo watapewa wale waliotayarishiwa."
Mark Swahili 10:41  Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia hayo, walianza kuchukizwa na Yakobo na Yohane.
Mark Swahili 10:42  Yesu akawaita, akawaambia, "Mnajua kwamba wale wanaofikiriwa kuwa watawala wa mataifa huwatawala watu wao kwa mabavu, na wakuu hao huwamiliki watu wao.
Mark Swahili 10:43  Lakini kwenu isiwe hivyo, ila anayetaka kuwa mkuu kati yenu, sharti awe mtumishi wenu.
Mark Swahili 10:44  Anayetaka kuwa wa kwanza, sharti awe mtumishi wa wote.
Mark Swahili 10:45  Maana Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, ila alikuja kutumikia, na kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi."
Mark Swahili 10:46  Basi, wakafika Yeriko, naye Yesu alipokuwa anatoka katika mji huo akiwa na wanafunzi wake pamoja na umati mkubwa wa watu, kipofu mwombaji aitwaye Bartimayo mwana wa Timayo alikuwa ameketi kando ya barabara.
Mark Swahili 10:47  Aliposikia kwamba ni Yesu wa Nazareti aliyekuwa anapita mahali hapo, alianza kupaaza sauti, "Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!"
Mark Swahili 10:48  Watu wengi walimkemea ili anyamaze, lakini yeye akazidi kupaaza sauti, "Mwana wa Daudi, nihurumie!"
Mark Swahili 10:49  Yesu alisimama, akasema, "Mwiteni." Basi, wakamwita huyo kipofu, wakamwambia, "Jipe moyo! Simama, anakuita."
Mark Swahili 10:50  Naye akatupilia mbali vazi lake, akaruka juu, akamwendea Yesu.
Mark Swahili 10:51  Yesu akamwuliza, "Unataka nikufanyie nini?" Huyo kipofu akamwambia, "Mwalimu, naomba nipate kuona."
Mark Swahili 10:52  Yesu akamwambia, "Nenda, imani yako imekuponya." Mara huyo kipofu akaweza kuona, akamfuata Yesu njiani.